• HABARI MPYA

    Monday, April 27, 2015

    MALINZI AWAOMBA TENGA, MSOLLA WAMSAIDIE NOOIJ TAIFA STARS

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewaomba wakufunzi wa ukocha nchini kumsaidia kocha wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij ili timu hiyo ifanye vizuri.
    Akizungumza wakati akifungua Semina ya Wakufunzi wa Ukocha wa madaraja ya juu nchini asubuhi ya leo katika ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Malinzi amesema kwamba Nooij yuko tayari kupokea maoni na ushauri wa wadau hao.
    Malinzi amesema kwamba si lazima wakufunzi hao wamuone moja kwa moja Nooij, lakini wanaweza kutafuta namna ambayo watamfikishia ujumbe kuhusu timu.
    Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi (kushoto) akiwatambulisha watu wa meza kuu, wakati wa ufunguzi wa kozi ya Wakufunzi wa ukocha

    Baadhi ya wakufunzi wakati wa ufunguzi
    Rais wa TFF, Tenga akiwa katika picha ya pamoja na Wakufunzi wa Makocha 

    “Unaweza kupitia kwa Mkurugenzi wa Ufundi (Salum Madadi), au Mayanga (Salum, kocha Msaidizi). Lengo ni kuboresha timu yetu ya taifa,” amesema Malinzi.
    Semina hiyo wakufunzi wa Makocha imeana rasmi leo na inatarajiwa kumalizika Mei 2 Mwaka huu ikiwajumuisha jumla ya makocha wakufunzi 21.
    Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Chilla Tenga, ambaye kwa sasa Mwenyekiti wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na Mjumbe wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ni miongoni mwa washiriki.
    Wengine ni kocha wa zamani wa Taifa Stars, Profesa Mshindo Msolla, Michael Bundala, George Komba, Oscar Don Korosso, Wilfred Kidao, Rogasian Kaijage, Mkisi Samson, Ally Mtumwa, Madaraka Bendera, Juma Nsanya,  Hamim Mawazo, Wanne Mkisi, Meja Abdul Mingange, Dk. Jonas Tiboroha, Nasra Mohamed, John Simkoko, Juma Mgunda, Triphonia Temba, Ambonisye  Florence, na Eugen Mwasamaki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AWAOMBA TENGA, MSOLLA WAMSAIDIE NOOIJ TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top