• HABARI MPYA

    Saturday, April 18, 2015

    SIMBA SC TAABAN MBEYA, YAPIGWA 2-0 NA MBEYA CITY

    Na Princess Asia, MBEYA
    MATUMAINI ya Simba SC kurudi kwenye michuano ya Afrika mwakani, leo yameanza kuyeyuka baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
    Matokeo hayo, yanaifanya Simba SC ibaki na pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 22, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 42 za mechi 22.  Yanga SC wapo kileleni kwa pointi zao 46, baada ya kucheza mechi 21.
    Mbeya City ilipata bao lake la kwanza dakika za majeruhi kipindi cha kwanza, mfungaji Paul Nonga aliyemalizia pasi ya Deus Kaseke iliyompita beki Mganda, Juuko Murusheed.
    Mbeya City wameifunga Simba SC mabao 2-0 Sokoine leo

    Katika mchezo huo, Simba SC ilipata pigo dakika ya 23, baada ya beki wake tegemeo, Hassan Isihaka kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mganda, Joseph Owino.
    Isihaka, beki anayeinukia vizuri aliumia baada ya kugongana na Peter Mapunda. 
    Mbeya City ilipata bao lake pili dakika ya 69, mfungaji Peter Mwalyanzi, aliyemalizia krosi Nonga aliyekuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Simba leo.
    Kikosi cha Mbeya City kilikuwa: Hannington Kalyesebula, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Christian Sembuli, Juma Nyoso, Kenny Ally, Peter Mapunda/Hassan Kibopile dk77, Raphael Daud, Paul Nonga, Cossmas Freddy/Peter Mwalyanzi dk59 na Deus Kaseke. 
    Simba SC: Peter Manyika, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Nassor Masoud ‘Chollo’, Juuko Murusheed, Hassan Isihaka/Joseph Owino dk23, Abdi Banda, Jonas Mkude, Elias Maguli/Issa Abdallah dk56, Ibrahim Hajibu, Said Ndemla na Ramadhani Singano ‘Messi’.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC TAABAN MBEYA, YAPIGWA 2-0 NA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top