• HABARI MPYA

    Monday, April 27, 2015

    TAIFA STARS KUWEKA KAMBI ETHIOPIA KWA AJILI YA MISRI KUFUZU AFCON

    RATIBA YA MECHI ZA KUNDI G

    Jumamosi Juni 13, 2015
    Nigeria v Chad
    Misri v Tanzania
    Jumamosi Sept 5, 2015
    Tanzania v Nigeria
    Chad v Misri
    Ijumaa Machi 25, 2016
    Chad v Tanzania
    Nigeria v Misri
    Jumatatu Machi 28, 2016
    Tanzania v Chad
    Misri v Nigeria
    Jumamosi Juni 4, 2016
    Chad v Nigeria
    Tanzania v Misri
    Jumamosi Sept 3, 2016
    Nigeria v Tanzania
    Misri v Chad
    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, itaweka kambi Addis Ababa, Ethiopia mwezi ujao kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Kundi G dhidi ya Misri, kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon. 
    Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewaambia Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam kwamba, lengo la kwenda kuweka kambi huko ni kufuata mazingira mazuri na hali ya hewa kwa ujumla.
    “Baada ya kupangwa kundi moja na Chad, Misri na Nigeria, Watanzania wengi kwa kweli wamekata tamaa kwamba hatuwezi kufanya vizuri. Lakini nimemuambia kocha (Mart Nooij) afanye kazi awashangaze watu,”amesema Malinzi.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi kushoto
    Rais huyo wa TFF amesema kwamba wataweka kambi ya muda mrefu Ethiopia na baada ya hapo watakwenda kucheza na Misri kwa matumaini makubwa.
    Malinzi amesema kwamba watahakikisha wanaiandaa vizuri timu ili iweze kutimiza ndoto za kurejea kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika, ambazo mara ya kwanza na ya mwisho ilicheza mwaka 1980.
    Aidha, Malinzi amewaomba wakufunzi wa ukocha nchini kumsaidia kocha Nooij ili timu hiyo ifanye vizuri.
    Akizungumza wakati akifungua Semina ya Wakufunzi wa Ukocha wa madaraja ya juu nchini asubuhi ya leo katika ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Malinzi amesema kwamba Nooij yuko tayari kupokea maoni na ushauri wa wadau hao.
    Malinzi amesema kwamba si lazima wakufunzi hao wamuone moja kwa moja Nooij, lakini wanaweza kutafuta namna ambayo watamfikishia ujumbe kuhusu timu.
    “Unaweza kupitia kwa Mkurugenzi wa Ufundi (Salum Madadi), au Mayanga (Salum, kocha Msaidizi). Lengo ni kuboresha timu yetu ya taifa,” amesema Malinzi.
    Semina hiyo wakufunzi wa Makocha imeana rasmi leo na inatarajiwa kumalizika Mei 2 Mwaka huu ikiwajumuisha jumla ya makocha wakufunzi 21.
    Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Chilla Tenga, ambaye kwa sasa Mwenyekiti wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na Mjumbe wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ni miongoni mwa washiriki.
    Taifa Stars itaweka kambi Ethiopia kujiandaa na Misri Juni mwaka huu

    Wengine ni kocha wa zamani wa Taifa Stars, Profesa Mshindo Msolla, Michael Bundala, George Komba, Oscar Don Korosso, Wilfred Kidao, Rogasian Kaijage, Mkisi Samson, Ally Mtumwa, Madaraka Bendera, Juma Nsanya,  Hamim Mawazo, Wanne Mkisi, Meja Abdul Mingange, Dk. Jonas Tiboroha, Nasra Mohamed, John Simkoko, Juma Mgunda, Triphonia Temba, Ambonisye  Florence, na Eugen Mwasamaki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS KUWEKA KAMBI ETHIOPIA KWA AJILI YA MISRI KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top