• HABARI MPYA

    Wednesday, April 15, 2015

    TANZANIA YANUKIA KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE, YAPANGWA TENA NA ZAMBIA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    TANZANIA itaanza na Zambia katika mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za mabinti chini ya umri wa miaka 20 mjini Papua, Guinea mwaka 2016.
    Kwa mujibu wa Ratiba ya mashindano hayo iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya droo yake kupangwa leo Cairo, Misri, Tanzania itaanzia moja kwa moja raundi ya kwanza.
    Hayo ni matokeo ya kupanda kwa soka ya wanawake Tanzania- na sasa timu zetu hazianzii Raundi ya Awali.
    Mchezo wa kwanza utafanyika Tanzania kati ya Julai 10,11 na  12 wakati marudiano yatakuwa Lusaka kati ya Julai 24, 25 na 26.

    Iwapo itafanikiwa kuitoa Zambia, Tanzania itafuzu moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia wanawake U20.
    Katika Raundi ya Awali, Djibouti itamenyana na  Burkina Faso, DRC na Gabon, Sierra Leone na Liberia mechi za kwanza zikichezwa kati ya Mei 1, 2 na 3 na marudiano Mei 15, 16 na  17 mwaka 2015.
    Mechi nyingine za Raundi ya Kwanza ni kati ya Cameroon na Ethiopia, Equatorial Guinea na Mali, Ghana na Senegal. 
    Baada ya hapo, mshindi kati ya DRC na Gabon atamenya na Sierra Leone, mshindi kati ya Sierra Leone na Liberia atamenyana na Nigeria na Afrika Kusini na Botswana.
    Mwishoni mwa wiki, timu ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars iliitoa Zambia katika kufuzu Michezo ya Afrika itakayofanyika Kongo Brazzaville mwishoni mwa mwaka kwa jumla ya mabao 6-5, baada ya kushinda 4-2 ugenini na kufungwa 3-2 nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YANUKIA KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE, YAPANGWA TENA NA ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top