• HABARI MPYA

    Tuesday, April 14, 2015

    YANGA, AZAM NA STAND KUCHEZWA USIKU DAR

    Na Alex Sanga, MWANZA
    MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya wenyeji, Yanga SC dhidi ya Stand United ya Shinyanga itachezwa Aprili 21, mwaka huu kuanzia Saa 12:00 jioni, imeelezwa.
    Mkurugenzi wa benchi la ufundi wa Stand United Muhibu Kanu, ameiambia BIN ZUBEIRY mjini hapa leo kwamba, wamepewa taarifa na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) mechi hiyo itachezwa Jumanne jioni.
    Muhibu amesema kwamba, baada ya mechi na Yanga, watacheza na Azam FC Aprili 25 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Saa 1:15 usiku.

    Stand United ndani ya wiki mbili itakuwa na mechi tatu, kuanzia Jumamosi ya Aprili 18 na JKT Ruvu Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA, AZAM NA STAND KUCHEZWA USIKU DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top