• HABARI MPYA

    Sunday, May 03, 2015

    DE LA HOYA AKANDIA STAILI YA UPIGANAJI YA MAYWEATHER

    BINGWA wa zamani wa dunia na mwasisi wa Golden Boy Promotions, Oscar De La Hoya amesema hajavutiwa na upiganaji wa kukimbia kimbia wa Floyd Mayweather akishinda dhidi ya Manny Pacquiao jana ukumbi wa MGM Grand, Las Vegad jana.
    De la Hoya ambaye alipigwa na mabondia wote hao, Mayweather na Manny Pacquiao hapo hapo MGM Grand mjini Las Vegas enzi zake anapigana, amesema Mayweather hakuwatendea haki mashabiki.
    "Wazi sijavutiwa na upiganaji wa kujilinda wa Mayweather. Niite wa zamani, lakini napenda mashabiki wafaidi fedha zao (za viingilio) kwa kuangalia ngumi zinavyopigwa,"amesema.
    Floyd Mayweather ameendeleza rekodi yake ya kutopigwa katika mapambano 48 baada ya kumshinda kwa pointi asubuhi ya leo Manny Pacquiao, lakini mchezo wake wa kujihami zaidi haukuwavutia wengi baada ya raundi 12 za pambano.
    Mayweather poses with his welterweight belts - the one he was awarded for this latest victory is worth $1m
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DE LA HOYA AKANDIA STAILI YA UPIGANAJI YA MAYWEATHER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top