• HABARI MPYA

    Thursday, May 21, 2015

    KOCHA WA SIMBA AWASILI, MTIBWA WAMDAKA JUU KWA JUU

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mbelgiji Piet de Mol aliyekuwa anawania kurithi mikoba ya Goran, amewasili leo Dar es Salaam na kwenda kukaa meza moja na Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser.
    Mtibwa walimtumia usafiri de Mol Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, ambao ulimpeleka kwenye ofisi za Mratibu wake, Jamal Bayser, barabara ya Nyerere.
    Mara moja Mtibwa wakafanya mazungumzo na kocha huyo na taarifa za awali zinasema wamemalizana, kilichobaki ni klabu huyo bingwa ya zamani nchini yenye maskani yake, Turiani, Morogoro kutangaza ndoa hiyo na Mbelgiji huyo.
    Piet de Mol akiwasili Uwanja wa Ndege wa JNIA, Dar es Salaam leo
    Kocha de Mol kulia amewa mezani kwa mazungumzo na Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser leo

    Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 60 ambaye ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka Afrika, Asia na Ulaya anaweza kuwa bosi wa kocha Mkuu wa sasa Mtibwa, Mecky Mexime.
    Mwaka jana, Piet de Mol alikuwa nchini Ghana akifanya kazi kama Mkurugenzi wa Ufundi wa akademi mjini Kumasi
    Mbali na Ghana ambako alifanya kazi na Asante Kotoko, De Mol amefundisha timu pia kwao Ubelgiji, Dubai, Qatar na China. Alikuwa kocha Msaidizi wa AA Gent kuanzia mwaka 1997 hadi 2001.
    Ilibaki kidogo Mbelgiji huyo arithi mikoba ya Mserbia, Goran Kopunovic klabu ya Simba SC ambayo awali ilishindwa kufikia makubaliano ya Mkataba mpya na kocha huyo aliyetaka kiwango cha fedha.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe aliiambia BIN ZUBEIRY wiki iliyopita kwamba Kopunovic alitaka dola za Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 100) kama dau la kusaini Mkataba na dola 8,000 (Sh. Milioni 16).
    Lakini sasa Kopunovic, aliyeiongoza Simba SC katika mechi 24 tangu aanze kazi Januari mwaka huu kati ya hizo, timu imeshinda mechi 18, sare mbili na kufungwa nne, amekubali kurudi kazini Msimbazi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA WA SIMBA AWASILI, MTIBWA WAMDAKA JUU KWA JUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top