• HABARI MPYA

    Sunday, May 03, 2015

    LEWIS: TATIZO WATU HAWAKUONA DAMU, ILA MAYWEATHER NI MTAALAMU

    BINGWA asiyepingika wa zamani wa dunia uzito wa juu, Lennox Lewis amesema Floyd Mayweather ni mtaalamu mkubwa wa ngumi.
    "Watu wengine wanataka kuona damu, wanachukizwa wasipoziona. Lakini haiondoi ukweli kwamba Floyd ni mtaalamu mkubwa,"amesema Muingereza huyo.
    Akizungumzia uwezekano wa pambano la Amir Khan na Mayweather, anasema; "Khan ni bondia, anatembea vizuri miguu yake. Kitu pekee ambacho Khan hana ni uzoefu mkubwa na ninahisi kwamba anaweza,"amesema Lewis.
    Mayweather is now unbeaten in 48 fights after producing a boxing masterclass against his rival

    Bingwa mwingine wa zamani wa uzito wa juu, David Haye amemtetea Mayweather. "Sanaa ya ngumi ni kupiga bila kupigwa. Mapambano 48 bila kupoteza kwa Money ni uthibitisho wa ubora wake,"amesema.
    Haye amesema pambano la marudiano baina ya waili linaweza kutokea na ndilo litamaliza ubishi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LEWIS: TATIZO WATU HAWAKUONA DAMU, ILA MAYWEATHER NI MTAALAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top