• HABARI MPYA

    Monday, May 04, 2015

    RAIS JK AWAPA 'TANO' YANGA SC KWA KUKOMAA NA WAARABU TUNISIA

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto) akiwa na viongozi na wachezaji wa Yanga SC Uwanja wa Ndege wa Dubai usiku huu. Rais Kikwete alikuwa anasubiri kuunganisha ndege kwenda Marekani, wakati Yanga SC walikuwa wanarejea nyumbani wakitokea Tunisa ambako jana walicheza na Etoile du Sahel ya huko na kufungwa bao 1-0 katika hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam. 

    Rais Kikwete aliwapongeza Yanga SC kwa kuonyesha ushindani dhidi ya Waarabu hao jana

    Inaaminika Rais Kikwete ni mpenzi na mwanachama hao wa Yanga SC

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS JK AWAPA 'TANO' YANGA SC KWA KUKOMAA NA WAARABU TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top