• HABARI MPYA

    Sunday, May 24, 2015

    WAMBURA SASA BOSI WA BODI YA LIGI

    Boniface Wambura kushoto amepewa majukumu mapya Bodi ya Ligi
    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini kuanzia tarehe 01, Juni 2015.
    Wambura kabla ya uteuzi huo alikua mkurugenzi wa mashandano TFF.
    TFF inampongeza Wambura kwa uteuzi na inaamini atatoa mchango mzuri katika kukuza na kuzitangaza ligi zetu.
    Kamati ya utendaji imemteau Martin Chacha (mratibu wa timu za Taifa) kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashandano TFF.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAMBURA SASA BOSI WA BODI YA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top