Getty
BEKI wa AC Milan, Alessandro Nesta
ametangaza kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu na kwenda kucheza nje
ya Ulaya, Marekani ikipewa kipaumbele.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36
anayecheza beki ya kati, ambaye mkataba wake Milan unaisha Juni, atakamilisha
miaka 10 ya kuwatumikia The Rossoneri, aliojiunga nao akitokea Lazio mwaka 2002
kwa dau la euro Milioni 30.5.
Amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia
Juventus, lakini amesema kwamba hatacheza tena Ulaya kutokana na kuamini hatamudu
tena kasi ya soka ya Ulaya kwa umri wake.
"Soka ya Italia na Ulaya ni ya kasi
sana hivi sasa kwangu," alisema kwenye mkutano na Waandishi wa Habari.
"Kama sitaona muhimu, ni bora nibaki nyumbani.
"Nimeshinda vitu vingi sana, lakini
kwa heshima kwa klabu na wachezaji wenzangu, nimeamua kujaribu uzoefu mwingine
katika klabu ambayo nitaweza kufanya vizuri."
Tangu awasili San Siro, Nesta ameisaidia Milan
kutwaa mataji mawili ya Serie A na mawili ya Ligi ya Mabingwa na mengineyo.


.png)
0 comments:
Post a Comment