![]() |
Mabingwa wa Coa Coca Cola, Morogoro |
Na Prince Akbar
KOMBAINI ya
Tanzania ya Copa Coca-Cola imeshika nafasi ya pili katika kambi ya kimataifa ya
michuano hiyo inayoendelea jijini Pretoria, Afrika Kusini. Tanzania imemaliza
mechi za kambi hiyo kwa kufikisha pointi 14.
Ilicheza
mechi yake ya mwisho jana (Septemba 5 mwaka huu) dhidi ya Malawi na kutoka
suluhu, matokeo yaliyoifanya ifikishe pointi 14. Zambia ndiyo iliyokamata
nafasi ya kwanza kwa kufikisha pointi 15.
Mechi hizo
zilichezwa kwa mtindo wa ligi baada ya nchi nyingine kushindwa kwenda Afrika
Kusini kutokana na kuchelewa kupata viza za kuingia za kuwawezesha kuingia
nchini humo.
Mbali ya
Tanzania, nchi nyingine zilizowahi kambi hiyo ni Kenya, Uganda, Nigeria,
Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia na timu mchanganyiko katika kambi hiyo
(CEWA).
Katika mechi
zake Tanzania ilitoka suluhu na Nigeria, ikafungwa 3-2 na Kenya, ikaichapa
Zimbabwe 3-0, ikailaza CEWA 3-0, ikaifunga Msumbiji 2-0, ikashinda 2-0 dhidi ya
Uganda na ikafungwa 1-0 na Zambia.
Wachezaji
wawili wa Tanzania wamechaguliwa kwenye kombaini ya kambi hiyo (Dream Team).
Wachezaji hao ni mfungaji bora Basil Seif ambaye ana mabao sita na kipa bora
Tumaini Baraka. Pia Sylvester Marsh wa Tanzania amechaguliwa kuwa kocha bora
katika kambi hiyo.
Makocha watano
kutoka timu ya Chelsea ya Uingereza wanaanza kutoka mafunzo leo (Septemba 6
mwaka huu) ambapo yatamalizika kesho (Septemba 7 mwaka huu) na timu zitarejea
nyumbani Septemba 8 mwaka huu. k.
Robert Luke
Udberg, Russel William Banyard, Oliver Staurt Woodall, Shane Jason Hughes na
Dean Aaron Steninger kutoka Chelsea FC Foundation ndiyo wanaounda jopo hilo la
makocha.
0 comments:
Post a Comment