Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya
LUIS NANI KWAHERI MANCHESTER UNITED, ANAWEZA KUBEBA VIRAGO VYAKE LEO
Zenit St Petersburg inatumai kukamilisha usajili wa pauni Milioni 25 wa winga wa Manchester United, Nani, mwenye umri wa miaka 25, kabla ya kufungwa pazia la usajili la Urusi leo.
Tottenham iko tayari kumto kwa mkopo kiungo wa England, Jermaine Jenas, mwenye umri wa miaka 29, akacheze Daraja la Kwanza ili kujihakikishia nafasi ya kucheza mechi.
Hull City na Huddersfield zote zina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Sunderland, Fraizer Campbell kwa mkopo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipandishwa kucheza Ligi Kuu akicheza kwa mkopo Hull mwaka 2008.
Mshambuliaji wa Manchester United, Josh King, mwenye umri wa miaka 20, ameionya klabu hiyo kwamba yupo tayari kuondoka Januari kama hatapata nafasi ya kucheza japo mechi kadhaa.
AVB AMPA MAZOEZI MAALUM ADEBAYOR
Kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas amempangia mazoezi maalum Emmanuel Adebayor, mwenye umri wa miaka 28, ili awe fiti na kuanza kuitumikia Tottenham katika mechi za mwanzoni za msimu.
Stefan Oakes, mwenye umri wa miaka 33, kiungo ambaye alishinda Kombe la Ligi akiwa na Leicester City na kucheza mechi zaidi ya 60 za Ligi Kuu, anaweza kutimkia Spalding United, ambayo inachesa Ligi Kuu ya United Counties.
Lyon ya Ufaransa inajaribu kuingilia kati usajili wa kiungo mwenye umri wa miaka 30, Joey Barton kutoka QPR kwenda Marseille - lakini wadhamini wao wanakwamisha.
JUVE WAMNANGA BENDTNER
Mshambuliaji Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka 24, ambaye amesajiliwa Juventus kwa mkopo wa msimu wa muda mrefu kutoka Arsenal wiki iliyopita, ameambiwa hayuko katika hali nzuri kimchezo ya kuchezea Kibibi Kizee hicho cha Turin.
0 comments:
Post a Comment