Manchester United hatimaye imethibitisha kusajili kinda la umri wa miaka 18, Angelo Henriquez. Mshambuliaji huyo wa Chile alifanyiwa vipimo vya afya katika klabu hiyo mwezi uliopita, kwa ajili ya uhamisho wa pauni Milioni 4, lakini usajili wake ulichelewa kuthibitishwa.
Nyota huyo wa Amerika Kusini anatua Old Trafford kutoka klabu ya Universidad ya Chile, ambako alifunga mabao 11 katika mechi 17 mwaka 2012 na kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa taifa lake.
Angelo Henriquez akikabidhiwa jezi ya Manchester United
Angelo Henriquez rasmi ametua Manchester United kwa pauni Milioni 4
Henriquez amekuwa na klabu hiyo tangu mwezi wote uliopita
0 comments:
Post a Comment