Mtakatifu Tom akiwanoa vijana |
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA wa
Yanga, Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji amesema kwamba timu yake iko imara sasa
tayari, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Septemba 15, mwaka huu, ingawa
anaendelea kutafuta mechi moja zaidi ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa ligi
hiyo.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY leo, Mtakatifu Tom alisema kwamba katika mazoezi yanayoendelea
sasa, anawakosa wachezaji wanne, ambao Hamisi Kiiza aliye na timu yake ya taifa
ya Uganda, Nurdin Bakari ambaye ni majeruhi, Salum Telela na Said Mohamed ambao
wanaumwa Malaria.
Kuhusu mchezo
wa kirafiki, Kavishe alisema kwamba amekwishawasilisha ombi lake hilo kwa
uongozi wa klabu na bado anasubiri jibu.
Kocha Saintfiet anajivunia rekodi ya
kushinda mechi 10 kati ya 11 alizoiongoza timu hiyo tangu ajiunge nayo miezi
miwili iliyopita.
Katika mechi hizo, sita zilikuwa za
michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame ambazo
alishinda tano na kufungwa moja tu ya kwanza dhidi ya Atletico ya Burundi,
akiiwezesha Yanga kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo Julai mwaka huu,
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kuifunga Azam FC mabao 2-0 kwehye fainali,
ambayo yalitiwa kimiani na Hamisi Kiiza ‘Diego Milito’ na Said Bahanuzi ‘Spider
Man’.
Hiyo kwa
ujumla ilikuwa mara ya tano mfululizo, Yanga inatwaa Kombe hilo, baada ya awali
kuchukua mwaka jana, wakiifunga Simba katika fainali bao 1-0, Uwanja wa Taifa
mfungaji Kenneth Asamoah ambaye ametemwa, ingawa siku hiyo Kiiza pia alifunga
bao safi, ambalo refa alilikataa.
Yanga
ilichukua kwa mara ya kwanza Kombe hilo, mwaka 1975 ikiifunga tena Simba katika
fainali, mabao 2-0 wafungaji Sunday Manara ‘Computer’ na Gibson Sembuli (sasa
marehemu) Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Ikachukua
tena mwaka 1993, Uwanja wa Nakivubo, Kampala, Uganda kwa kuifunga SC Villa
mabao 2-1, yaliyotiwa kimiani na Said Nassor Mwamba ‘Kizota’ (sasa marehemu) na
Edibily Jonas Lunyamila.
Ilichukua
tena mwaka 1999, ikiifunga tena SC Villa, Uwanja wa Nakivubo, kwa penalti 5-3,
kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, Yanga ikisawazisha bao kupitia kwa
Lunyamila, baada ya Hassan Mubiru kutangulia kuifungia Villa, siku hiyo Manyika
Peter akicheza penalti mbili za Waganda.
Aidha, kwa
kutwaa Kombe hilo chini ya Mbelgiji huyo, Yanga imeendeleza rekodi yake ya
kutwaa mataji ya michuano hiyo, chini ya makocha wa kigeni watupu baada ya
mwaka 1975 kuchukua chini ya Tambwe Leya aliyekuwa raia wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kuchukua uraia wa Tanzania, (sasa
marehemu), 1993 chini ya Nzoyisaba Tauzany aliyekuwa raia wa Burundi kabla ya
kuchukua uraia wa Tanzania, mwaka 1999 chini ya Raoul Shungu wa DRC na mwaka
jana chini ya Mganda, Sam Timbe.
REKODI YA SAINTFIET YANGA
1.
Yanga
Vs JKT Ruvu 2-0
2.
Yanga
Vs Atletico (Burundi) 0-2
3.
Yanga
Vs Waw Salam (Sudan Kusini) 7-1
4.
Yanga
Vs APR (Rwanda) 2-0
5.
Yanga
Vs Mafunzo (Z’bar) 1-1 (5-3penalti)
6.
Yanga
Vs APR (Rwanda) 1-0
7.
Yanga
Vs Azam 2-0
8.
Yanga
Vs African Lyon 4-0
9.
Yanga
Vs Rayon (Rwanda) 2-0
10. Yanga
Vs Polisi (Rwanda) 2-1
11. Yanga
Vs Coastal Union 2-1
0 comments:
Post a Comment