![]() |
Geoffrey Nyange 'Kaburu' amejitoa |
Na Boniface Wambura
WANAMICHEZO
50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika
Februari 24 mwaka huu wamerejesha fomu hizo.
Waombaji
ambao hawakurejesha fomu ni Geofrey Nyange aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati
ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa
akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha
kamili ya waombaji ambao wamerejesha fomu ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi,
Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Michael Wambura, Ramadhan Nassib na
Wallace Karia (Makamu wa Rais).
Kwa upande
wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro Samson
(Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel
Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai
na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari
Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu
Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na
Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na
Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki
Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala,
Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na
Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin
Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
Wakati huo
huo: Waombaji wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo
uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha fomu.
Kwa upande
wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph Manji wa Yanga
wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.
Nafasi mbili
za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza zimeombwa na watu
watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa Moro United, Kazimoto
Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu Mwindadi.
Kamati ya
Uchaguzi ya TFF itaanza kukutana kesho kwa ajili ya kupitia fomu zote
zilizowasilishwa na waombaji kwa ajili ya uchaguzi wa TFF na ule wa Bodi ya
Ligi Kuu.
Pia Kamati
inapenda kuwakumbusha waombaji uongozi kuzingatia Kanuni za Uchaguzi, kwani
baadhi yao wameanza kufanya kampeni kupitia vyombo vya habari. Kwa walioanza
kufanya kampeni kabla ya wakati wanajiweka katika hatari ya kuenguliwa
kushiriki katika uchaguzi.