• HABARI MPYA

    Tuesday, August 05, 2014

    YANGA SC WATAKIWA KUMUWASILISHA MAXIMO TFF

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    YANGA SC wametakiwa kuwasilisha jina la kocha wao mpya, Mbrazil Marcio Maximo na wasaidizi wake.
    Hiyo imo katika agizo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuzitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha orodha ya watendaji wa mabenchi yao ya ufundi yakiongozwa na Kocha Mkuu.
    Jina la Marcio Maximo na wasaidizi wake yanatakiwa na TFF

    Ni wajibu wa klabu kuhakikisha zinatekeleza maagizo hayo kwani ni matakwa ya Kanuni za VPL na zile za FDL.
    Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itaanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu wakati ile ya FDL inatarajia kuanza Oktoba mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WATAKIWA KUMUWASILISHA MAXIMO TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top