• HABARI MPYA

    Sunday, November 09, 2014

    BAFETIMBI ATOKEA BENCHI NA KUIANGAMIZA ARSENAL ENGLAND

    ARSENAL imepata kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Swansea City Uwanja wa Liberty usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. 
    Alexis Sanchez aliifungia Arsenal bao la kuongoza dakika ya 63 akimalizia krosi ya Danny Welbeck, kabla ya Gylfi Sigurdsson kuwasawazishia wenyeji kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 30 dakika ya 75.
    Bafetimbi Gomis alirokwa benchi na kuingia uwanjani kuifungia Swansea bao la ushidi dakika ya 78.
    Kikosi cha Swansea kilikuwa: Fabianski, Rangel, Bartley, Williams, Taylor, Ki, Carroll/Britton dk87, Emnes/Barrow dk67, Sigurdsson, Montero na Bony/Gomis dk76. 
    Arsenal: Szczesny, Chambers/Sanogo dk90, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Ramsey (Walcott 79), Flamini/Wilshere dk80, Oxlade-Chamberlain, Sanchez, Cazorla na Welbeck. 
    Bafetimbi Gomis (wa pili kushoto) akiruka juu dhidi ya mabeki wa Arsenal kuifungia Swansea bao la ushindi

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2827375/Swansea-2-1-Arsenal-Bafetimbi-Gomis-heads-dramatic-winner-two-minutes-coming-complete-turnaround-hosts.html#ixzz3Ib1LkXLE 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAFETIMBI ATOKEA BENCHI NA KUIANGAMIZA ARSENAL ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top