Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
BALOZI wa Hispania nchini Tanzania, Luis Guesta amesema kwamba udhamini wa Castler Lager kwa FC Barcelona ndiyo umefungua milango ya ziara ya mabingwa hao wa zamani wa Ulaya nchini.
Nyota waliowika FC Barcelona miaka kadhaa ya nyuma, wapo nchini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya nyota wa zamani wa Tanzania leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na wachezaji wote waliokuja walialikwa katika hafla ya vinywaji na vitafunwa iliyofanyika usiku wa jana nyumbani kwa Balozi Guesta, Masaki, Dar es Salaam.
Balozi huyo amesema kwamba udhamini wa Castler Lager, kama kampuni ya kwanza ya Afrika kuidhamini Barcelona, matunda yake ni ziara hiyo.
“Napenda kutumia fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Castle Lager, wadhamini wa Barcelona. Udhamini wao ndiyo umesababisha leo Barcelona wapo Tanzania,”alisema.
Balozi huyo alisema anatarajia mchezo mzuri leo baina ya magwiji wa Barcelona na Tanzania Eleven, kwa sababu wachezaji wa timu zote mbili ni wazuri na wa kihistoria.
Kwa upande wake, Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks ambaye naye alihudhuria hafla hiyo kwa sababu ya wachezaji wa Kiholanzi wanaochezea Barcelona alisema kwamba amefurahi juu ya ziara hiyo na anawapongeza Castle Lager kwa kufanya jambo kubwa.
“Barcelona ni timu yenye wapenzi duniani kote. Watanzania kupata fursa ya kuwaona wachezaji wa timu hii kubwa ni jambo zuri na la kihistoria,”alisema.
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Johan Cruyff kwa upande amewaahidi Watanzania burudani nzuri ya kandanda uwanjani.
“Tumeambiwa kuhusu Real Madrid (magwiji). Walipokuja hapa walishinda. Sasa na sisi lazima tushinde, kwa sababu wale (Real Madrid) ni wapinzani wetu,” amesema.
Cruffy amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na hilo watalidhihirisha uwanjani jioni ya leo. “Leo jioni tumetoka kwenye mazoezi yetu ya mwisho na hakuna tatizo katika kikosi chetu, mtawaona nyote wote mlioambiwa, wapo,”amesema.
Nyota mwingine wa zamani wa Barca aliyekuja na kikosi cha magwiji, Luis Garcia alisema amefurahi kuja Tanzania na jioni ya leo atawapa burudani nzuri ya sika safiu Watanzania watakaojitokeza Uwanja wa Taifa.
Castle Lager, inayotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzana (TBL) iliingia Mkataba wa kuidhamini Barcelona mwaka 2013 na Agosti 16 mwaka huo ukafanyika uzinduzi wa udhamini huo kwa Tanzania.
Udhamini huu, umeifanya Castle Lager kuwa Bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika hususani hapa Tanzania na nchi nyingine 10 barani Afrika ambapo Castle Lager imekuwa kinywaji rasmi pia kwenye shughuli zote za klabu ya FC Barcelona katika nchi hizi.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa FC Barcelona kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya Kiafrika jambo ambalo limewafungulia njia mashabiki wa FC Barcelona nchini Tanzania na nchi nyingine barani kuweza kupata bidhaa, matukio ya kukumbukwa, ikiwemo ziara hii na nafasi za kushinda safari ya kwenda Barcelona Hispania kuitembelea klabu hiyo.
Castle Lager imekuwa ikijihusisha na soka barani Afrika kwa muda wa miaka 85 ambapo hivi sasa inadhamini ligi za soka katika nchi za Zimbabwe, Swaziland na Lesotho. Castle Lager pia ni mdhamini wa mashindano ya COSAFA yanayofanyika Kusini mwa Afrika na CECAFA yanayofanyika Afrika Mashariki.

![]() |
| Kutoka kulia ni Luis Garcia, Balozi wa Hispania nchini, Luis Guesta, Johan Cruyff na balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks wakati wakiwakabidhi Mabalozi hao jezi za Barcelona katika hafla hiyo. |
![]() |
| Hapa wanagongesha glasi zao katika hafla hiyo |
![]() |
| Kulia ni Meneja Masoko wa TBL, Arthur Kanza, katikati Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo, Kevin O'Flaherty na Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo |
“Napenda kutumia fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Castle Lager, wadhamini wa Barcelona. Udhamini wao ndiyo umesababisha leo Barcelona wapo Tanzania,”alisema.
Balozi huyo alisema anatarajia mchezo mzuri leo baina ya magwiji wa Barcelona na Tanzania Eleven, kwa sababu wachezaji wa timu zote mbili ni wazuri na wa kihistoria.
Kwa upande wake, Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks ambaye naye alihudhuria hafla hiyo kwa sababu ya wachezaji wa Kiholanzi wanaochezea Barcelona alisema kwamba amefurahi juu ya ziara hiyo na anawapongeza Castle Lager kwa kufanya jambo kubwa.
“Barcelona ni timu yenye wapenzi duniani kote. Watanzania kupata fursa ya kuwaona wachezaji wa timu hii kubwa ni jambo zuri na la kihistoria,”alisema.
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Johan Cruyff kwa upande amewaahidi Watanzania burudani nzuri ya kandanda uwanjani.
“Tumeambiwa kuhusu Real Madrid (magwiji). Walipokuja hapa walishinda. Sasa na sisi lazima tushinde, kwa sababu wale (Real Madrid) ni wapinzani wetu,” amesema.
Cruffy amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na hilo watalidhihirisha uwanjani jioni ya leo. “Leo jioni tumetoka kwenye mazoezi yetu ya mwisho na hakuna tatizo katika kikosi chetu, mtawaona nyote wote mlioambiwa, wapo,”amesema.
Nyota mwingine wa zamani wa Barca aliyekuja na kikosi cha magwiji, Luis Garcia alisema amefurahi kuja Tanzania na jioni ya leo atawapa burudani nzuri ya sika safiu Watanzania watakaojitokeza Uwanja wa Taifa.
![]() |
| Meneja Kiwanda wa TBL, Calvin Martin kulia na Maofisa wengine mbalimbali waliohudhuria hafka hiyo wakifuatilia hotuba mbalimbali fupi |
![]() |
| Waalikwa wakifurahia matukio mbalimbali katika hafla hiyo |
![]() |
| Watu wanatafuna vitu vidogo vidogo vilivyoandaliwa kwenye hafla hiyo |
Castle Lager, inayotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzana (TBL) iliingia Mkataba wa kuidhamini Barcelona mwaka 2013 na Agosti 16 mwaka huo ukafanyika uzinduzi wa udhamini huo kwa Tanzania.
Udhamini huu, umeifanya Castle Lager kuwa Bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika hususani hapa Tanzania na nchi nyingine 10 barani Afrika ambapo Castle Lager imekuwa kinywaji rasmi pia kwenye shughuli zote za klabu ya FC Barcelona katika nchi hizi.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa FC Barcelona kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya Kiafrika jambo ambalo limewafungulia njia mashabiki wa FC Barcelona nchini Tanzania na nchi nyingine barani kuweza kupata bidhaa, matukio ya kukumbukwa, ikiwemo ziara hii na nafasi za kushinda safari ya kwenda Barcelona Hispania kuitembelea klabu hiyo.
Castle Lager imekuwa ikijihusisha na soka barani Afrika kwa muda wa miaka 85 ambapo hivi sasa inadhamini ligi za soka katika nchi za Zimbabwe, Swaziland na Lesotho. Castle Lager pia ni mdhamini wa mashindano ya COSAFA yanayofanyika Kusini mwa Afrika na CECAFA yanayofanyika Afrika Mashariki.

.png)
0 comments:
Post a Comment