• HABARI MPYA

    Saturday, April 18, 2015

    CHELSEA WAIKALISHA UNITED DARAJANI, UBINGWA HUOO

    BAO pekee la winga Mbelgiji Eden Hazard limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Stamford Bridge, London.
    Ushindi huo unazidi kuisogeza karibu na taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England The Bleus ya Jose Mourinho, baada ya kufikisha pointi 76 kutokana na mechi 32.
    United inabaki na pointi zake 65 baada ya kucheza mechi 33 na inaendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya Arsenal yenye pointi 66 za mechi 32, mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City yenye pointi 61 za mechi 32.   
    Hazard alifunga bao hilo pekee dakika ya 38 akimalizia kazi ya nzuri Mbrazil, Oscar. Mshambuliaji wa Man United, Radamel Falcao alilalamika kuchezewa rafu ya makusudi na Nahodha wa Blues, John Terry.
    Hazard alikaribia kufunga bao la pili kama asingegongesha mwamba kufuatia pasi ya Didier Drogba. Kiungo wa United, Ander Herrera alionyeshwa kadi ya njano kwa kujiangusha dakika ya 95 akitafuta penalti. 
    Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Terry, Cahill, Azpilicueta, Zouma, Matic, Oscar/Ramires dk67, Fabregas/Mikel dk92, Hazard/Willian dk93 na Drogba.
    Manchester United: De Gea, Valencia, Smalling, McNair, Shaw/Blackett dk80, Rooney, Mata/Januzaj dk70, Ander Herrera, Fellaini, Young/Di Maria dk70 na Falcao.
    A TV camera gets a close-up of the goalscorer as Hazard celebrates with Didier Drogba in front of a section of home fans at Stamford Bridge
    Hazard akishangilia na Didier Drogba mbele ya mashabiki wao Uwanja wa Stamford Bridge

    PICHA ZAIDI NENDA
    : 
    http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3044957/Chelsea-1-0-Manchester-United-Eden-Hazard-strikes-Jose-Mourinho-s-men-step-Premier-League-title.html#ixzz3XgmkIGiB 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA WAIKALISHA UNITED DARAJANI, UBINGWA HUOO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top