![]() |
| Nassor Bin Slum (katikati) akicheza kiduku kushangilia ushindi wa Coastal Union leo Chamazi |
Ikitoka kufungwa mabao 8-0 na Yanga SC, Coastal leo ilikuwa timu tofauti Chamazi, ikicheza soka maridadi na kupata ushindi muhimu wa ugenini.
Mabao ya Coastal yamefungwa na Rama Salim na Iker Obinna na sasa mabingwa hao wa Ligi Kuu 1988 wanafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 23 na wanapanda hadi nafasi ya sita kutoka ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Bin Slum alitangaza kurejea Coastal mapema wiki hii kufuatia matokeo mabaya mfululizo kiasi cha kuibuka hofu ya kushuka daraja, lakini bahati mbaya, mchezo wa kwanza, timu hiyo ikalala 8-0 kutoka Yanga SC kabla ya kuzinduka leo.
Leo Bin Slum alikuwa mwenye furaha jukwaani, akiwa amejichanganya na mashabiki wakicheza ‘viduku’ kushangilia mabao na soka ‘iliyoshiba’.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo leo, Azam FC imetoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Ndanda imetoka sare ya 0-0 na Prisons Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara wakati mchezo kati ya Kagera Sugar na Ruvu Shooting uliokuwa uchezwe leo Shinyanga, umesogezwa mbele hadi Jumatatu.
![]() |
| Bin Slum a pili kushoto akiwa na manazi wenzake wa Coastal Chamazi leo |




.png)
0 comments:
Post a Comment