• HABARI MPYA

    Saturday, April 11, 2015

    MAYANGA AREJESHWA MTIBWA SUGAR KUOKOA JAHAZI

    Na Alex Sanga, MWANZA
    MTIBWA Sugar imemrejesha kocha wake wa zamani, Salum Mayanga awe Mshauri Mkuu wa Ufundi, baada ya kuona jahazi linaelekea kuzama katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mtibwa leo wanawakaribisha mabingwa watetezi, Azam FC katika mfululizo wa ligi hiyo, Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    Mayanga ambaye kwa sasa ni kocha Msaidizi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya Mholanzi Mart Nooij- sasa atakuwa anatumia muda ambao hana majukumu ya kitaifa kwenda kufanya kazi na mchezaji wake wa zamani, Mecky Mexime.
    Salum Mayanga amerejeshwa Mtibwa Sugar kuokoa jahazi

    Mexime ndiye kocha Mkuu wa Mtibwa kwa sasa na baada ya kuifikisha timu hiyo kwenye hatua ya kujinusuru kushuka daraja, anaongezewa nguvu. 
    Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba wamepania kupambana kuhakikisha hawashuki Daraja.
    "Wachezaji wetu wapo katika morali nzuri na wameahidi kushinda mechi dhidi ya Azam, lazima tushinde,” alisema Kifaru. Tukishnda michezo miwili kati ya sita iliyobaki, hatuwezi kushuka tena Daraja,"amesema Kifaru.
    Katika mchezo huo, Mtibwa itamkosa mchezaji wake, Mussa Chibwabwa kutokana na kuwa majeruhi.
    Kwa sasa Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 12 katika Ligi Kuu yenye timu 14, ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 20. Mwisho wa msimu, timu mbili zitashuka.
    Mtibwa iliuanza msimu vizuri na kuwa kileleni kwa robo yote ya mwanzo- kabla ya kuanza kuporomoka taratibu na sasa ipo ‘danger zone’.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAYANGA AREJESHWA MTIBWA SUGAR KUOKOA JAHAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top