• HABARI MPYA

    Friday, April 13, 2012

    JUVE WAPIGWA FAINI, ONYO KALI KWA UBAGUZI

    Mashabiki wa Juve
    VINARA wa Serie A, Juventus wamepigwa faini ya Euro fined 30 000 na onyo kali baada ya mashabiki wake kukutwa na hatia ya kufanya vitendo vya kibaguzi juzi wakishinda 2-1 nyumbani dhidi ya Lazio.
    Zomea ya kejeli za kibaguzi ilisikika sehemu tano katika mechi hiyo, lakini klabu hiyo na mashabiki wengine walijaribu kuzima hali hiyo, Serie A imesema katika taarifa yake.
    Juve ililazimika kucheza milango ya Uwanja wake imefungwa miaka mitatu iliyopita baada ya kumfanyia kejeli za kibaguzi, mshambujliaji wa Inter Milan wakati huo, Mario Balotelli.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JUVE WAPIGWA FAINI, ONYO KALI KWA UBAGUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top