• HABARI MPYA

    Friday, April 13, 2012

    KIONGOZI YANGA AFARIKI DUNIA

    MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Wakili Theonist Rutashoborwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake, Dar es Salaam.
    Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu ameaimbia bongostaz asubuhi hii kwamba bado wanawasiliana na familia ya marehemu ili kujua zaidi na saa 5:00 asubuhi watafanya Mkutano na Waandishi wa Habari.
    Rutta ni mwanachama ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa klabu hiyo kupata ufadhili wa Yussuf Manji mwaka 2006, kutokana na harakati alizoanzisha za Harambee ya Yanga kufuatia hali mbaya ya kifedha ndani ya klabu hiyo chini ya uongozi wa Francis Mponjoli Kifukwe enzi hizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIONGOZI YANGA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top