![]() |
Di Natale |
NAHODHA wa Udinese ya Italia, Antonio Di Natale amesemja
anaweza kustaafu mwishoni mwa msimu, kufuatia kifo cha mchezaji mwenzake wa
zamani, Piermario Morosini akiichezea Livorno Jumamosi.
Kijana wa umri wa miaka 25, Morosini, ambaye alikuwa
akicheza kwa mkopo kutoka klabu hiyo ya Serie A, Udinese, alizimia na kufariki
dunia baada ya kupata tatizo la moyo katika mechi ya Serie B huko Pescara.Jana, Di Natale alisema soka inachezwa sana Italia na kwa hilo; ''mwaka jana nilifikiria kustaafu. ... nitacheza hizo mechi sita za mwisho kwa Mario na kasha tutaona.''
Di Natale ana umri wa miaka 34. Mshambuliaji huyo wa Itali amekuwa mfungaji bora wa Serie A kwa misimu miwili iliyopita.
Kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa mabao yake 20, akizidiwa matatu tu na Zlatan Ibrahimovic wa AC Milan.
0 comments:
Post a Comment