• HABARI MPYA

    Tuesday, April 17, 2012

    MUAMBA AREJEA NYUMBANI

    Muamba katikati na viongozi wa Bolton pembeni yake
    KIUNGO wa England mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fabrice Muamba, ambaye nusura afe baada ya moyo wake kusimama ameruhusiwa kutoka hospitali ya London Chest na kurejea nyumbani.
    Muamba amekuwa akipokea matibabu katika hospitali ya moyo mjini London. Kiungo huyo wa Bolton Wanderers ya Ligi Kuu, alianguka uwanjani wakati klabu hiyo ikicheza na Tottenham katika Robo Fainali ya Kombe la FA.
    Amekuwa akisaidiwa na daktari aliyempa huduma ya kwanza alipoanguka uwanjani. Muamba amewaambia waandishi wa habari kwamba anatarajia kupata muda na familia yake huku akiwarudishia shukurani mashabiki na wenzake ambao waliungana naye wakati wote akiwa hospitalini.
    Hapo Jumamosi shirikisho la soka Italia lilisimamisha mechi zote baada ya mchezaji wa klabu ya Livorno, Piermario Morosini, kuzirahi na baadaye kufariki dunia alipokuwa akichezea klabu yake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUAMBA AREJEA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top