• HABARI MPYA

    Tuesday, April 17, 2012

    MUHIMU KUJUA HAYA KABLA YA BAYERN NA REAL LEO

    Robben wa Bayern
    Ronaldo wa Real
    WENYEJI Bayern Munich watawarejesha kwenye kikosi cha kwanza Philipp Lahm, Franck Ribery na Mario Gomez katika mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa leo dhidi ya Real Madrid, baada ya wachezaji hao kupumzishwa mwishoni mwa wiki timu yao ikitoka sare na Mainz.
    Bastian Schweinsteiger amerejea baad aya kutumikia adhabu ya mechi moja, lakini Jupp Heynckes amesema jana kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kwamba hana uhakika kama Nahodha huyo Msaidizi ataanza kwa sababu alikosa mazoezi ya kujiandaa na mechi hiyo.
    Toni Kroos anaweza kuwapo, wakati Luiz Gustavo anaweza kucheza kama kiungo wa pili wa ulinzi.
    Mabeki Daniel Van Buyten anayeumwa mguu na Breno (goti) wote watakuwa nje.
    Kocha wa Madrid, Jose Mourinho anatarajiwa kuwaanzisha pamoja Karim Benzema na Angel Di Maria baada ya wawili hao kukaa benchi Jumamosi timu yake ikishinda dhidi ya Sporting Gijon.
    Xabi Alonso amerejea baada ya kumaliza adhabu, lakini Ricardo Carvalho na Lassana Diarra wote bado majeruhi na hawatacheza.

    JE WAJUA?
    •Bayern Munich imeshinda mechi sikta mfululizo za Ligi ya Mabingwa nyumbani na imeshinda mechi 12 kati ya 13 za Ulaya Allianz Arena.
    •The Bavarian haijawahi kufungwa na na Real Madrid nyumbani (imeshinda nane na kutoa sare moja). Rekodi ya jumla ya Munich dhidi ya Madrid ni kushinda mechi 10, sare 2, kufungwa 6.
    •Klabu hizo awali zimekutana katika Nusu Fainali nne, huku Bayern ikishinda mara tatu (1976, 1987 na 2001) na Madrid moja tu mwaka 2000.
    •Jupp Heynckes, ambaye alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa akiwa mchezaji wakiitoa Madrid msimu wa 1997-98, hajawahi kuifunga timu ya Hispania katika mechin mbili tangu awe kocha.
    •Rekodi ya Real Madrid kutofungwa katika Ligi ya Mabingwa msimu huu na ikiwa imefungwa mabao sita tu, inawafanya wawe timu yenye ukuta bora zaidi katika timu zote zilizosalia kwenye michuano hii.
    •The Castilian wameshinda mechi moja tu katika ardhi ya Ujerumani katika mechi 22 (Kushinda 1, sare6, kufungwa 15) – ushindi pekee ukiwa wa 3-2 dhidi ya Bayer Leverkusen msimu wa 2000-01.
    •Madrid inaweka rekodi ya kucheza Nusu Fainali ya 23 katika michuano hiyo mikubwa Ulaya na inatarajiwa kucheza Fainali ya 13.
    •Cristiano Ronaldo ameifungia Real Hat Tricks 14 katika La Liga pekee, mbili zaidi dhidi ya Ferenc Puskas katika rekodi ya jumla ya klabu hiyo, lakini bado yuko nyumka ya rekodi ya Alfredo Di Stefano aliyefunga 22.

    VIKOSI VYA LEO:
    BAYERN MUNICH: Neuer, Lahm, Boateng, Badstuber, Alaba, Gustavo, Kroos, Robben, Muller, Ribery na Gomez.
    REAL MADRID: Casillas, Arbeloa, Pepe, Ramos, Marcelo, Khedira, Alonso, Di Maria, Ozil, Ronaldo na Benzema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUHIMU KUJUA HAYA KABLA YA BAYERN NA REAL LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top