• HABARI MPYA

    Saturday, April 14, 2012

    WALCOTT AWAKUMBUSHA KITU ARSENAL HAWAWEZI KUSAHAU MSIMU HUU

    Walcott katikati ya Song kulia na Sagna kushoto
    MUINGEREZA Theo Walcott amesema kwamba Arsenal ilianza ligi rasmi msimu huu baada ya kuifunga 5-3 Chelsea, Oktoba 29, mwaka jana.
    Ushindi huo ulikuja baada ya Arsenal kuuanza msimu vibaya ikiwemo kutandikwa mabao 8-2 na Manchester United.
    Walcott alicheza kwa kikubwa sana siku hiyo akiwa na jezi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, na akafunga bonge la bao lililodhihirisha kipaji na umahiri wake.
    Dogo huyo wa umri wa miaka 23 amezungumzia mechi hiyo kama moja ya mechi ambazo hawezi kuzisahau msimu huu na ndiyo iliyowafufua.
    "Mechi na Chelsea ilikuwa hatua kubwa kwa sababu tulijua tuko vizuri [wakati huo]," alisema Walcott.
    "Kwenda nje ya nyumbani na kufunga mabao mengi, ilikuwa ni kila kitu. Ilikuwa babu kubwa jinsi tulivyoshirikiana, baada ya mechi (furaha yake) ilikuwa kama tumetwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
    "Huo ni moja ya wakati ambao tunataka utokee tena na bahati nzuri umetokea tena katika wiki za karibuni."
    Walcott amefunga mabao manane katika timu yake hadi sasa msimu huu, mawili kati ya hayo alifunga kwenye ushindi wa 5-2 dhidi ya Spurs, Februari.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WALCOTT AWAKUMBUSHA KITU ARSENAL HAWAWEZI KUSAHAU MSIMU HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top