![]() |
Didier Drogba (wa tatu kushoto) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga kwenye Uwanja wa Wembley, London leo. Chelsea ikishinda 5-1 dhidi ya Spurs Nusu fainali ya FA |
KLABU ya Chelsea usiku huu imeitandika Tottenham Hotspur mabao
5-1 kwenye Uwanja wa Wembley na kutinga fainali ya Kombe la FA ambako
itamenyana na Liverpool.
Shukrani kwao Didier Drogba, Juan Mata, Ramires, Frank
Lampard na Florent Malouda waliofunga mabao hayo, yanayoiwezesha Chelsea kucheza
fainali ya nne ya Kombe la FA ndani ya miaka sita.Bao pekee la Tottenham lilifungwa na Gareth Bale.
Ushindi huo unakuja wakati Chelsea inaelekea kwenye mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona Uwanja wa nyumbani, Stamford Bridge Jumatano.
0 comments:
Post a Comment