• HABARI MPYA

    Saturday, April 14, 2012

    GUARDIONA AMTEMBELEA ABIDAL HOSPITALI, AKAA NAYE DAKIKA 20

    Abidal
    KOCHA wa Barcelona, Pep Guardiola amemtembelea beki Eric Abidal hospitali jana baada ya mchezaji huyo kufanyiwa upasuaji wa ini mapema wiki hii.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa amepigwa kisu na inasemekana anaendelea vizuri baada ya zoezi hilo gumu.
    Guardiola alitumia muda wa dakika 20 akiwa na Abidal na familia yake, na amemtakia mchezaji huyo kupona haraka katika upasuaji huo wa pili juu ya tatizo hilo.
    Rais wa Barcelona, Sandro Rosell alisema kwamba Mfaransa huyo anaendelea vizuri.
    Kwa sasa klabu hiyo Catalans inachuana vikali na wapinzani wao, Real Madrid katika mbio za ubingwa wa La Liga na leo inacheza na Levante
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GUARDIONA AMTEMBELEA ABIDAL HOSPITALI, AKAA NAYE DAKIKA 20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top