KLABU ya Manchester United imejiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya
England, kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa kwenye Uwanja wa Old
Trafford, Manchester.
Hadi mapumziko, Man United walikuwa mbele kwa mabao 2-0,
yaliyotiwa kimiani na Wayne Rooney kwa penalti dakika ya saba na Danny Welbeck dakika
ya 43.Rooney aliwainua tena vitini mashabiki wa Man U dakika ya 73 alipofunga bao la tatu na Nani akafunga la nne dakika ya 90.
United sasa ina pointi 82, baada ya kucheza mechi 34, sawa na wapinzani wao Man City wenye pointi 77.
Arsenal ni ya tatu kwa pointi zake 64, Spurs ya nne kwa pointi zake 59 sawa na Newcastle ya tano, wakati Chelsea yenye pointi 57 ni ya sita.
0 comments:
Post a Comment