Aden Rage |
SIKU chache baada ya kuwepo kwa
utata juu ya ujio wa klabu yaTp Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC) kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki na klabu ya Simba, uongozi wa
Simba umewatoa hofu mashabiki wa Simba na wa soka kwa ujumla juu ya ujio huo.
Hivi karibuni aliyewahi kuwa
mdhamini wa Simba na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo Azim
Dewji alitangaza kuileta Tp Mazembe kwa ajili ya kuipa makali Simba ambayo
inatarajiwa kucheza mechi ya kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy ya
Sudan.
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail
Aden Rage ameiambia mamapipiro blogspot leo kuwa
yeye na makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Azim Dewji
wamekuwa wakifanya mawasiliano ya mara kwa mara na mmliki wa TP Mazembe Mose
Katumbi.
Alisema anashangazwa na taarifa
zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari zikimnukuu kocha msaidizi wa Tp
Mazembe Lamine Ndiaye kutokuwa na
taarifa za ziara hiyo kitu ambacho hakina mantiki yoyote kwa kuwa kocha kazi
yake ni kufundisha tu.
“Kama mtu anataka uhakika awasiliane
na Katumbi ama katibu wake Kitenge, sisi tunafanya mazungumzo wenyewe kwa
wenyewe (viongozi) na mambo yakiwa tayari wanapewa taarifa wengine ndiyo maana
hata baadhi ya viongozi wenzangu wea Simba hawana taarifa rasmi,”Alisema Rage.
Rage aliongeza kuwa mipango
kuhusiana na ujio wa timu hiyo ambayo nayo inatarajiwa kukwaana na El Mereikh
ya Sudan katika Ligi Ya mabingwa barani Afrika yanakwenda vema na kama kutakuwa
na mabadiliko yoyote watatoa taarifa rasmi.Katika hatua nyingine, Rage
amempongeza Dewji kwa kutimiza ahadi yake ya kuwakabidhi wachezaji wa timu hiyo
kitita cha shilingi milioni 15 baada ya kuitoa Es Setif ya Algeria na kutinga
hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF).
0 comments:
Post a Comment