![]() |
Kipre Tchetche wa Azam kulia |
Na Princess Asia
AZAM FC imekubali matokeo ya kutolewa katika Kombe la BankABC Sup8R na imewapongeza Simba SC sababu timu yao ya vijana ni nzuri.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga alisema jana kwamba, bahati ilikuwa yao Simba SC, kwani nafasi mbili walizopata walizitumia vizuri kwa kufunga mabao yao yaliyowapeleka fainali.
Jaffar alisema kwamba jana bahati haikuwa upande wa Azam, kwani walipoteza nafasi za wazik za kufunga mabao zaidi ya tano.
“Mtu kama Kipre Tcheche peke yake, alipoteza nafasi nne za wazi kabisa za kufunga akiwa amebaki yeye na kipa, lakini hiyo ndiyo soka na sisi tumekubali matokeo.
Tunawapongeza Simba SC, tunarudi kambini kuanza kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii, ambayo tutacheza tena na Simba,”alisema.
Wakati jana Simba ilicheza timu ya vijana na Azam ilitumia wachezaji wengi wa akina, Mechi ya Ngao timu zote zinatarajiwa kushusha vikosi vyake kamili vya Ligi Kuu.
Mara ya mwisho, vikosi kamili vya timu hizo vilikutana kwenye mechi ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mwezi uliopita na Simba ilichapwa mabao 3-0, yote yakitiwa kimiani na John Raphael Bocco ‘Adebayor’, ambaye kwa sasa yupo Afrika Kusini akifanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu ya Super Sport United.
0 comments:
Post a Comment