![]() |
Mecky Mexime |
Na
Princess Asia
KOCHA wa Mtibwa Sugar
ya Morogoro, Mecky Mexime amesema kwamba ana matumaini ya kuwafunga
Simba B na kubeba na Kombe la Bank ABC katika fainali itayapopigwa keshokutwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na BIN
ZUBEIRY jana, Mecky alisema kwamba amewaona Simba wakati wanaitoa Azam kwa
kuichapa 2-1 ni wazuri na wanacheza kwa uelewano sana, lakini Jumamosi anaamini
atawafunga tu.
“Kabla sijawa kocha wa
Mtibwa ya wakubwa, nilikuwa kocha wa vijana, na nilikuwa pia kocha wa vijana wa
Morogoro katika Copa Coca Cola, ambayo ilikchukuja ubingwa. Kwa hiyo nawajua
vijana, hivyo vijana wa Simba hawanipi hofu,”alisema Mecky.
Mexime alisema anajua
namna ya kuwapoteza vijana uwanjani na kuvuna ushindi, tena wa mabao ya kutosha
kabisa,
Mtibwa Sugar ilitinga
Fainali kwa kishindo, kwa kuinyuka Jamhuri ya Pemba, mabao 5-1, ambayo yalitiwa
kimiani na Babu Ally Seif dakika ya 15, Salvartoy Ntebe dakika ya 17, Mfaume
Shaaban aliyejifunga dakika ya 38, Vincent Barnabas dakika ya 43 na Awadh Juma
dakika ya 85 wakati la kufutia machozi la Jamhuri lilifungwa na Mbarouk Chande
dakika ya 62.
Hadi sasa, Mtibwa ndio timu pekee ambayo haijapoteza pointi
hata moja kwenye mashindano hayo baada ya kushinda mechi zake zote tatu za Kundi
B, 2-1 dhidi ya Polisi Moro, 2-0 dhidi ya Azam na 5-0 dhidi ya Super Falcon na
jana 5-1 dhidi ya Jamhuri katika Nusu Fainali.
Simba B yenyewe ilitoa sare moja tu ya kufungana 1-1 na
Jamhuri katika mchezo wa kwanza, lakini mechi zake nyingine ilizifunga 2-0 kila
timu, Mtende na Zimamoto ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment