• HABARI MPYA

    Monday, September 17, 2012

    SZCZESNY BADO KASEJA WA ARSENAL, ASEMA WENGER


    Wojciech Szczesny, Arsenal
    Szczesny
    Arsene Wenger amesema kwamba Wojciech Szczesny ataendelea kuwa namba moja Arsenal hata baada ya kufanya makosa katika mechi ambayo Gunners iliiripua Southampton.
    Szczesny, alirejea milingotini baada ya kukosa mechi mbili kutokana na kuwa majeruhi, na akafungwa bao la kizembe na Southampton, ambalo lilikuwa pekee lililofungwa na Danny Fox .
    Pamoja na hayo, kipa huyo kinda akarejesha imani kwa kocha wake na Wenger amesema Szczesny ataendelea kulinda lango la Gunners.
    "Wojciech ni namba 1, vinginevyo nibadili mawazo yangu. Hiyo iko sahihi. Ndiyo maana amerejea langoni.
    "Huwezi kubadili kipa kila wakati anapofanya makosa madogo, kwa sababu ukiiwa na makipa watatu wabaya. Kujiamini kunahitajika."
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SZCZESNY BADO KASEJA WA ARSENAL, ASEMA WENGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top