![]() |
Mkurugenzi wa mMasoko wa kampuni ya bia Serengeti, Ephraim Mafuru akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo katika hoteli ya JB Belmenote kuhusu kampeni za Tupo Pamoja |
Machi 14, 2013, JB BELMONTE, DAR ES SALAAM: Leo katika hafla iliyohudhuriwana waandishi wa habari, wageni na wadau mbalimbali Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni mpya na ya kipekee inayoenda kwa kauli mbiu ya TUPO PAMOJA. Katika hafla hiyo iliyofana asubuhi ya leo pia ilihudhuriwa na wadau wa bia hii katika ishara ya kushereheka mafanikio na shangwe za bia hii.
Akiongea na waandishi wa habari asubuhi la yeo, Mkurugenzi wa mMasoko wa kampuni ya bia Serengeti, Ephraim Mafuru alisema kwamba, “ kwa miaka kumi saa, tumeona na kushuhudia ukuaji na mafanikio makubwa”. Bia hii inajulikana kwa kampeni ya ‘raha kamili kwa wengi wanaifahanu kama Chui. Pia kwa udhamini wa Taifa stars ambao uliinua hadhi ya soka la Tanzania kwa kiwango kikubwa. Kuna ufadhili wa Fiesta, ambao wote mnajua mchango Fiesta inatoa katika ukuaji wa tasnia ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini. Aliendelea Bw. Mafuru
![]() |
Meneja wa bia ya Serengeti, Allan Chonjo kulia akizungumza pembeni ya Mafuru |
“Tunawakaribisha wote katika hafla mbali mbali ambazo tutaandaa ili kueneza kampeni hii ya Tupo Pamoja kama mlivyoona katika matangazo niliyowaonyesha, tutaleta shangwe popote mlipo., Alieleza meneja wa kinywaji hicho Bw. Allan Chonjo, baada ya kuonyesha matangazo mbali mbali yatakovyokuwa katika vyombo vya habari.
Hafla hiyo ya uzinduzi pia ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Kampuni ya bia ya Serengeti wakiwemo wasambazaji wa bia. Kampeni hii inawatambua na kuwathamini watanzania wote kwa mafanikio yao katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Kampuni ya bia ya bia ya Serengeti inajihusisha na biashara ya vinjwaji vyenye vileo kama bia- Premium Serengeti Lager, Tusker Lager, Tusker Malt Lager, Tusker Lite, Uhuru Peak Lager, Pilsiner, Guinness na vinywaji vikali kama Johnnie Walker, Smirnoff Vodka, Richot, Bond 7 and Gilbeys. Pia vinywaji visivokuwa na kileo kama Malta Guinness.
![]() |
Mafuru katika picha tofauti akizungumza leo kuhusu kampeni hiyo |