• HABARI MPYA

    Sunday, March 10, 2013

    SIMBA SC ILIVYOTAFUNA WAGOSI WA KAYA LEO TAIFA

    Mrisho Khalfan Ngassa wa Simba SC, akiruka kwanja la beki wa Coastal Union ya Tanga, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba SC ilishinda 2-1.

    Mrisho Ngassa akishangilia kwa staili ya aina yake, baada ya kufunga bao la kwanza

    Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba SC, akimiliki mpira pembeni ya beki wa Coastal Union, Mbwana Hamisi

    Philip Mugenzi wa Coastal Union akimdhibiti Rashid Ismail wa Simba SC

    Haruna Chanongo wa Simba SC akimtoka beki wa Coastal Union, Hamad Hamisi

    Kipa wa Coastal Union, Shaaban Kado akidaka mpira wa juu

    Amri Kiemba wa Simba SC akipasua katikati ya wachezaji wa Coastal Union

    Salim Kinje wa Simba SC kulia, akijaribu kumpokonya mpira mchezaji wa Coastal Union, Mohamed Athumani

    Kipa wa Simba, Abbel Dhaira akidaka mpira wa juu 

    Beki wa Simba SC, Miraj Adam kulia akitibiwa na Daktari wa timu yake baada ya kuumia katika moja ya hekaheka za mchezo huo

    Ukisikia patashika ndio hii, Amri Kiemba wa Simba SC kushoto ameanguka chini jirani na mpira na Hamad Hamisi wa Coastal Union pia naye kaanguka. Juu ni Mrisho Ngassa wa Simba akiupigia hesabu mpira

    Kipa wa Coastal Union,Shaaban Kado amedaka mpira mwili mwa Mrisho Ngassa wa Simba SC aliyeangukia kushoto. Kulia ni beki wake Mbwana Hamisi akiwa tayari kutoa msaada.

    Kikosi cha Simba SC leo

    Kikosi cha Coastal Union leo

    Beki wa Simba SC, Shomary Kapombe akijipoza na baradu baada ya kuumia 

    Muda wa shangwe; Wachezaji wa Simba SC wakishangilia bao la pili lililofungwa na Haruna Chanongo 

    Haruna Chanongo wa Simba SC akienda chini baada ya kukwatuliwa na Philip Mugenzi wa Coastal Union

    Haruna Chanongo akipambana...

    Haruna Chanongo wa Simba SC akifumua shuti mbele ya Hamad Hamisi wa Coastal Union 

    Haruna Chanongo akikosa bao la wazi, baada ya kuwatoka mabeki wa Coastal  na kumzidi maarifa kipa Shaaban Kado, lakini mpira ulienda nje

    Mrisho Ngassa akiwatoka mabeki wa Coastal...

    Mrisho Ngassa akimiliki mpira pembeni ya kiungo wa Coastal, Razack Khalfan

    Haruna Chanongo akimiliki mpira kwa uhodari wa hali ya juu, zamani ilikuwa ikiitwa kapiga kizungu. kushoto ni beki wa Coastal, Hamad Hamisi

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA SC ILIVYOTAFUNA WAGOSI WA KAYA LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top