![]() |
Messi |
Messi alitumbukiza mkwaju wake
wa penalti dakika ya 72 na kuipa Barcelona ushindi wa 2-1 na kumfikia Ronaldo, ambaye
aliweka rekodi hiyo kwa bao la dakika ya 74 la kichwa katika ushindi wa Real
Madrid wa 3-1 dhidi ya Sporting Gijon.
Madrid imeendelea kuongoza La
Liga kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya mabingwa watetezi mara tatu, Barcelona
kabla ya mechi baina ya timu hizo, maarufu kama El Clasico wiki ijayo, ambayo
itatoa picha yam bio za ubingwa msimu huu zikiwa zimebaki mechi nne ligi
kufikia tamati.
0 comments:
Post a Comment