• HABARI MPYA

    Sunday, April 15, 2012

    ROSICKY: TUMEWAKATAMATA MASHABIKI WETU EMIRATES

    Rosicky kushoto na Alex Song
    NYOTA wa Arsenal Tomas Rosicky amesema kwamba tayari sasa wameungana na mashabiki wao kwenye Uwanja wa Emirates na wamejenga imani.
    Kwa ujumla, Arsenal imekuwa ikifanya vizuri katika mechi za nyumbani msimu huu, ikiwa imepoteza mechi tatu tu katika mashindano yote na na kufunga mabao 24 katika mechi zao saba zilizopita.
    Rosicky anaamini mashabiki wamechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo na kiwango kizuri cha Arsenal na anaamini kwa pamoja wanaweza kufanya Emirates iwe kiota chao cha shangwe.
    “Siku za karibuni mapokeo yamekuwa mazuri katika mechi zetu za nyumbani – timu inayoweza kuhisi hilo na ni msaada mkubwa kwetu,”alisema.
    “Ni hisia nzuri kuwa na mashabiki ambao wako nyuma yako kwa dakika zote 90.
    “Kwa kweli mashabiki wanatufanya tufanye tofauti kwenye Uwanja wa Emirates na tunatumai tutadumisha muungano huu kwa kuendeleza wimbi la ushindi zaidi.”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROSICKY: TUMEWAKATAMATA MASHABIKI WETU EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top