![]() |
Fabio |
Beki huyo wa Kibrazil mara
kadhaa amekuwa akipelekwa kikosi cha wachezaji wa akiba msimu huu katika siku
za karibuni, lakini amecheza mechi moja tu ya Ligi Kuu England, tena akiingia
kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Patrice Evra katika ushindi wa 5-0 dhidi ya
Wolves.
Kocha anahofia kijana huyo
mwenye umri wa miaka 21 anahitaji uhakika wa kucheza katika umri wake mdogo na
yuko tayari kumpeleka klabu nyingine kwa msimu wa 2012/2013.
Baada ya kucheza fainali ya Ligi
ya Mabingwa dhidi ya Barcelona msimu uliopita, beki huyo wa pembeni amecheza
mechi 15 tu msimu huu, nyingi kati ya
hizo zikiwa za Ulaya au Kombe la Ligi.
"Natumai kwamba Fabio ataendelea
vema kama pacha wake [Rafael] na, kumsaidia, atakwenda kucheza kwa mkopo msimu
ujao kumpa uzoefu wa kucheza kikosi cha kwanza," alisema kocha katika safu
yake maalum leo.
"Tayari nimekwishazungumza
naye na anatambua thamani ya kucheza kwa uhakika katika kiwango cha juu, kuliko
nafasi ambayo tunampa hivi sasa."
0 comments:
Post a Comment