• HABARI MPYA

    Tuesday, May 22, 2012

    DROGBA AANGUA KILIO, MACHOZI DEBE AKIWAAGA WACHEZAJI WENZAKE CHESLEA


    Didier Drogba
    Didier Drogba akipunga mkono wake kwa ishara ya kwaheri baada ya Chelsea kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Published: 21st May 2012

    DIDIER DROGBA alibubujikwa na machozi wakati akiwaambia wachezaji wenzake: ‘Naondoka.’

    Mshambuliaji huyo hatari amesema inamuuma moyoni kufikia tamati ya miaka minane ya kuwa na Chelsea.
    Drogba alizungumza huku analia wakati anawaambia John Terry, Frank Lampard na wengineo: ‘Hatutakuwa pamoja tena msimu ujao.’
    Alitoa tamko hilo la kushitua katika sherehe za ubingwa wa Blues, saa 24 baada ya kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, anatarajiwa kuungana na mchezaji mwenzake aliyekuwa naye Chelsea,  Nicolas Anelka katika klabu ya Shanghai ya China kwa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki.
    Lakini uhamisho huo umeingia shaka jana usiku, baada ya kuibuka habari, kocha Anelka amekwaruzana na wamiliki wa klabu hiyo ya Shanghai.
    Drogba alisema: “Ingawa ni miaka  mitatu sasa tangu niseme nataka kuondoka, inaniwia vigumu kukubali nimefikia mwisho na klabu hii — hususan tangu nikatae mwisho huu.”
    Drogba aliliambia jarida la Ufaransa: “Nisingeweza kujiona nimekaa benchi nawaangalia wachezaji wengine wanacheza, wakati klabu inapanga kujenga timu mpya.
    Anelka amesaidia mawasiliano kati ya Shanghai na Drogba kufikia sehemu n zuri.
    Lakini Mfaransa huyo, hafurahishwi na hali ya mambo anayokabiliana huko tangu avue dakluga zake na kukaa kwenye benchi la ufundi, akirithi mikoba ya Jean Tigana mwezi uliopita na anaweza kuamua kuondoka.


    REKODI YA DROGBA CHELSEA:

    • MECHI YA KWANZA: v Manchester United, Agosti 15, 2004
    • BAO LA KWANZA: v Crystal Palace, Agosti 24, 2004
    • IDADI YA MECHI ALIZOCHEZA: 342
    • MABAO ALIYOFUNGA: 157
    • MATAJIPremier League: 2004-05, 2005-06, 2009-10; FA Cup: 2006-07, 2008-09, 2009-10, 2011-12; League Cup: 2004-05, 2006-07 Champions League: 2011-12
    • UFUNGAJI BORA LIGI KUU: 2007, 2010
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DROGBA AANGUA KILIO, MACHOZI DEBE AKIWAAGA WACHEZAJI WENZAKE CHESLEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top