![]() |
Rachel kulia, enzi za uhai wake akiwa na 'babe' Princess Asia Mahmoud katika ofisi za New Habari, Sinza Kijiweni, Dar es Salaam. |
MWANDISHI mwandamizi wa habari za michezo,
sanaa na burudani Tanzania, Rachel Mwiligwa amefariki dunia jana katika hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa
matibabu.
Hadi anafariki dunia, Rachel alikuwa Mhariri
wa habari za michezo wa gazeti la Mtanzania, linalotolewa na kampuni ya New
Habari 2006 Limited.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari Ltd,
Hussein Mohamed Bashe ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi hii kwamba wameipokea kwa
masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanadada huyo, aliekuwa m chapakazi hodari
na akasema; “Ni pigo kubwa kwetu kama kampuni, pigo kwa wana habari, ni pigo
kwa tasniya ya habari kwa ujumla, tumempoteza mtu muhimu, aliyekuwa mchapakazi
hodari,”alisema Bashe.
Bashe alisema taarifa zaidi kuhusu msiba
huo na utaratibu wa mazishi, zitatolewa baadaye- baada ya uoongozi wa kampuni hiyo,
kuzungumza na ndugu wa marehemu.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.
0 comments:
Post a Comment