![]() |
Mbwana Samatta |
MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Ally Samatta amenusurika kufa kwa ajali ya gari leo mjini Lubumbashi,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Samatta anayechezea Tout Puissant Mazembe,
ameiambia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba alikoswakoswa na gari la abiria leo asubuhi.
“Nipeni pole na mie, maana nimekoswa koswa
leo asubuhi na gari ya abiria, sidhani kama ningeomba hata maji,”alisema.
Aidha, Samatta amesema baada ya kunusurika
na kifo, kuanzi leo atakuwa anasali sala tano. “Kuanzia leo, nitakuwa wa kwanza
masjid,”alisema.
Samatta pia amesikitishwa na kifo cha kiungo
wa Simba, Patrick Mutesa Mafisango na amewapa pole wapenzi wa SImba na familia
ya marehemu.
Samatta ameiambia BIN ZUBEIRY kutoka
Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kifo hicho kimesmshitua
sana, lakini hana budi kukubali kwa kuwa ni kazi ya Mungu.
“Dah majonzi tena, poleni familia ya
Patrick Mutesa, poleni Simba SC, poleni wapenzi wa soka Tanzania, hatuna jinsi,
Mungu ndio mpangaji wa yote,”alisema.
Mafisango alifariki dunia usiku wa kuamkia
leo, eneo la Tazara, Dar es Salaam kwa ajali ya gari.
Vyanzo vimesema alikuwa anatoka Maisha Club
disko na akiwa katika eneo hilo alikutana na mwendesha pikipiki aliyeingia ovyo
na katika kumkwepa alijikuta anatoka barabarani na kuingia mtaroni na kupoteza
maisha.
0 comments:
Post a Comment