TIMU ya soka ya vijana ya Azam
FC, maarufu kama Azam Academy leo inacheza mechi ya kukamilisha ratiba kwenye
michuano ya Rollingston inayoendelea nchini Burundi, katika mechi ambayo mgeni
rasmi atakuwa rais wa Burundi, Perre Nkurunziza.
Azam tayari imekwishafuzu Robo
Fainali, baada ya kushinda mechi zake mbili za awali 1-0 dhidi ya Kyazanga FC
ya Uganda na 3-0 dhidi ya Nyirakongo Academy ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC).
Katika mchezo huo, kikosi cha
Azam kinatarajiwa kuwa; Aishi, Mgaya, Shabalala, Dizana, Mkomola, Reyna,
Mudathiri, Kaijage, Machuppa, Kelvin na Kimwaga.
Simba na Yanga zilialikwa pia kwenye michuano hiyo,
ila zote zimejitoa dakika za mwishoni. |
0 comments:
Post a Comment