Na Prince Akbar
KAMPUNI ya bima ya Maxinsure imetoa vifaa vya mazoezi kwa
timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) vyenye thamani ya sh.
milioni 1.3.
Vifaa hivyo ambavyo ni jezi, bukta na soksi 20, vizibao
(bibs) 20 na mipira miwili vimekabidhiwa leo (Julai 12 mwaka huu) kwa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo,
Amisa Juma.
Akikabidhi vifaa hivyo, Amisa amesema wamefanya hivyo ikiwa
ni sehemu ya mchango wao kwa jamii lakini vilevile wameamua kuiunga mkono timu
hiyo ambayo wanajua haina mdhamini kutokana na vipaji na uwezo ambao umekuwa
ukioneshwa na wachezaji wake.
Pia amezitaka kampuni, taasisi, watu binafsi na Serikali
kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali
inayotarajia kushiriki.
0 comments:
Post a Comment