Na Prince Akbar
KOCHA wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet amewaacha kwenye kikosi
kitakachoshiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame kuanzia Jumamosi wachezaji watatu nyota na chipukizi, Omega Seme, Simon Msuva
na Frank Damayo kwa sababu watakuwa na majukumu ya kitaifa kwa muda mrefu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu, makao makuu
ya klabu makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Saintfiet
alisema kwamba wachezaji hao watakuwa na timu ya taifa ya vijana chini ya umri
wa miaka 20, inayojiandaa mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa
ya Afrika Julai 29 dhidi ya Nigeria.
Mtakatifu Tom anasoma majina |
“Kwa mujibu wa kanuni
natakiwa kuwaachia wachezaji siku tano kabla ya mechi, na Jumamosi wanacheza na
Rwanda, Jumatatu wanarudiana na Rwanda, baada ya hapo watakuwa kwenye maandalizi
ya mechi na Nigeria, kwa hivyo sitakuwa nao hata kwenye Nusu Fainali, kwa
sababu hiyo nimeamua kuwaacha,”alisema.
Saintfiet alisema amemtema pia Nahodha wa klabu hiyo,
Nsajigwa Shadrack katika kikosi cha wachezaji 20, lakini amesema mchezaji huyo
ni muhimu na atakuwa naye kwenye Ligi Kuu.
Amewataja wachezaji aliowateua baada ya kushauriana na
wasaidizi wake, Freddy Felix Minziro na Mfaume Athumani kuwa ni; makipa Yaw Berko
na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, David Luhende, Kelvin Yondan,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua, Stefano
Mwasyika, viungo Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’,
Haruna Niyonzima, Shamte Ally, Nizar Khalfan, Idrisa Assenga, Hamisi Kiiza na
washambuliaji Said Bahanuzi na Jerry Tegete.
Yanga, ambao ndio mabingwa watetezi wa Kagame, watafungua
dimba na mabingwa wa Burundi, Atletico FC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
KIKOSI CHA YANGA
KAGAME;
Makipa; Yaw Berko
na Ally Mustafa ‘Barthez’
Mabeki; Juma Abdul,
David Luhende, Kelvin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Godfrey Taita, Ladislaus
Mbogo, Oscar Joshua na Stefano Mwasyika
Viungo; Athumani Iddi
‘Chuji’, Rashid Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Shamte Ally, Nizar
Khalfan na Idrisa Assenga.
Washambuliaji;
Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Jerry Tegete.
Mtakatifu Tom akizungumza na Waandishi hapo |
0 comments:
Post a Comment