• HABARI MPYA

    Wednesday, December 05, 2012

    HANS POPPE AJA KAMPALA KWA MAMBO MAWILI MAKUBWA, WANAOSEMA SIMBA IMEFULIA WANAJIDANGANYA

    Hans Poppe 

    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe anatarajiwa kutua mjini hapa kesho, kwa ajili ya mambo mawili makubwa, usajili wa wachezaji na kocha mpya, atakayerithi mikoba ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana kwa simu kutoka Dar es Salaam, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) anakuja Kampala kufanya kazi za Simba SC.
    Ingawa Hans Poppe hakutaka kuzugumzia kwa undani ujio wake hapa, lakini BIN ZUBEIRY inatambua anakuja kufanya mazungumzo na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri na wachezaji kadhaa waliowavutia katika mashindano haya, akiwemo mshambuliaji Mganda Brian Umony.
    Lakini pia, Hans Poppe anakuja kumalizana na mshambuliaji wao Mganda, Emmnanuel Okwi ambaye amemaliza mkataba wake.
    Vyombo vya habari Dar es Salaam vimeripoti kuwa, Okwi atasaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi Simba SC kwa dau la dola za Kimarekani 40,000 pamoja na nyongeza ya mshahara.      
    Okwi amekuwa akihusishwa na habari za kuhamia Yanga na Azam FC baada ya kumaliza mkataba wake Simba SC, lakini wakati huo huo inaelezwa amekwishafikia makubaliano na Wekundu wa Msimbazi kuongeza mkataba.
    Kwa upande wa kocha wa timu ya taifa ya Malawi, iliyotolewa katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwa kufungwa na Kenya 1-0 jana, tayari Phiri amekwishasema yupo tayari kufanya kazi Simba SC na inaelezwa mazungumzo ya awali yamekwishafanyika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HANS POPPE AJA KAMPALA KWA MAMBO MAWILI MAKUBWA, WANAOSEMA SIMBA IMEFULIA WANAJIDANGANYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top