• HABARI MPYA

    Wednesday, December 05, 2012

    INJINI YA THE CRANES YAOMBA JEZI YA NIYONZIMA YANGA HARAKA

    Oloya
    I
    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    KIUNGO wa Uganda, Moses Oloya amesema kwamba yupo tayari kuachana na klabu yake, Saigon Xuan Thanh ya Vietnam na kujiunga na Yanga SC ya Dar es Salaam, ambao watampa maslahi mazuri.
    Yanga SC inamfuatilia mchezaji huyo katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwa ajili ya kumsajili, akazibe pengo la kiungo wake Mnyarwanda, Haruna Niyonzima anayetakiwa na El Merreikh ya Sudan.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Uwanja wa Mandela, Namboole baada ya kuiongoza nchi yake, kuifunga Ethiopia mabao 2-0, Oloya alisema kwamba kama Yanga watafika Kampala na kuzungumza naye, wakiafikiana atahamishia maisha yake Dar es Salaam.
    “Nimebakiza mkataba wa mwaka mmoja katika klabu yangu, lakini tukikubaliana naweza kuondoka Vietnam bila masharti magumu, Yanga waje tu tuzungumze,”alisema.
    Kiongozi mmoja wa Yanga, jana aliiambia BIN ZUBEIRY kwa simu jana kutoka Dar es Salaam kwamba, wanafuatilia maendeleo ya Oloya katika michuano hiyo na iwapo ataendelea kufanya vizuri watakuwa tayari kumsajili.
    “Unajua Haruna ana asilimia kubwa ya kuondoka, sasa lazima tupate kiungo mbadala mzuri kama yeye na mzoefu, tumefuatilia kwa haraka haraka tumemuona huyu Oloya, ngoja tuendelee kumuangalia,”alisema kiongozi huyo.  
    Oloya alizaliwa Oktoba 22, mwaka 1992 na kabla ya kujiunga na Saigon Xuan Thanh mwaka 2010, aliichezea KCC ya nyumbani kwao tangu mwaka 2009. Kiungo huyo alianza kuichezea Uganda mwaka jana na sasa amekuwa tegemeo la timu hiyo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: INJINI YA THE CRANES YAOMBA JEZI YA NIYONZIMA YANGA HARAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top