• HABARI MPYA

    Monday, December 10, 2012

    KATONGO AJA KUWAPA SHUGHULI MABEKI STARS

    Katongo

    Na Prince Akbar
    KOCHA Mkuu wa timu ya Zambia, Chipolopolo, ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
    Kwa mujibu wa Chama cha Soka Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
    Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KATONGO AJA KUWAPA SHUGHULI MABEKI STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top