![]() |
Kanumba |
MSICHANA mmoja aliyetambulika
kwa jina la Mariam Elias, mkazi wa Misugusugu wilayani Kibaha, mkoani hapa,
amenusurika kupoteza maisha yake baada ya kunywa sumu ya panya, kutokana na
kifo cha msanii mahiri wa filamu hapa nchini, Stephen Kanumba.
Kwa mujibu wa mamapipiro.blogspot
Ofisa Habari wa Shirika la Elimu Kibaha, Rose Mtei, alisema kwamba, msichana
huyo alifikishwa katika hospitali Teule ya Tumbi jana usiku, majira ya saa
5:30, akiwa na hali mbaya kutokana na sumu aliyokunywa.
Mtei alisema kwamba, msichana
huyo wakati alipofikishwa hospitalini hapo, hali yake ilikuwa ni mbaya, lakini
madaktari waliyokuwa zamu, waliweza kujitahidi kwa hali na mali kumuhudumia kwa
lengo la kuokoa maisha yake.
“Ni kweli katika hospitali yetu
ya Tumbi, usiku wa tarehe 10 majira ya saa 5:30, tuliweza kumpokea msichana
huyo ambaye alikuwa amekunywa sumu ya panya na alipoulizwa, alisema ni kutokana
na kifo cha nguli wa tasnia ya filamu hapa nchini, Stephen kanumba,” alifafanua
Mtei.
Aidha, Mtei alisema kwamba, inasemekana
msichana huyo alikuwa akimpenda sana marehemu Kanumba kutokana na umahiri wake
katika kuigiza filamu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.
Ofisa huyo aliongeza kuwa, kwa
sasa msichana huyo baada ya kupatiwa matibabu na madaktari, anaendelea vizuri
na kwamba, bado yupo katika uangalizi kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi zaidi.
Kanumba alifariki dunia usiku wa
kuamkia Jumamosi iliyopita nyumbani kwake Sinza Vatican kutokana na ugomvi wa
kimapenzi, kifo kilichowagusa maelfu ya mashabiki na wadau wa filamu wa rika
mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment